Chimala – 16 Novemba 2025
Katika Ibada maalum iliyofanyika Usharika wa Chimala, KKKT Dayosisi ya Kusini imemsimika rasmi Mchungaji Veronica Enock Mbilinyi kuwa Mkuu wa Jimbo la Chimala. Tukio hili la kihistoria lilihudhuriwa na viongozi wakuu wa makanisa, wachungaji wa sharika mbalimbali, pamoja na waumini kutoka sehemu mbalimbali za jimbo hilo.
Ibada hiyo iliongozwa na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mhashamu Dk.George Mark Fihavango. Viongozi wengine waliojiunga na ibada hiyo ni Mkuu wa Seminari ya Kilutheri ya Kidugala, Mchungaji Wallace Lupenza pamoja na wachungaji wa Sharika za Chimala.