Huduma ya Uinjilisti Jimbo la Chunya

KAZI YA UINJILISTI JIMBO LA CHUNYA – KKKT Dayosisi ya Kusini
Tarehe: 01–10 Agosti 2025 

Utangulizi
Katika kutekeleza wito wa huduma ya kiroho na kushiriki Habari Njema ya wokovu kwa jamii, Uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya kusini, uliandaa mpango wa Uinjilisti kwenye la Chunya kuanzia Tarehe 01/08/2025 hadi 10/08/2025. Dayosisi ya kusini kupitia uongozi wake madhubuti chini ya Askofu Daktari George Mark Fihavango, Uongozi wa dayosisi kupitia Idara ya Uinjilisti na Misioni ikiongozwa na msaidizi wa Askofu Daktari Johnson Gudaga, umeonesha mshikamano na ari ya kutimiza agizo la Bwana Yesu Kristo: “Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi…” (Mathayo 28:19). Huduma hii pia ilikuwa na uzito wa kipekee kwa Askofu wa Dayosisi ya Kusini, ambaye alitumia tukio hili kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 tangu alipopewa daraja la uchungaji.

Mkuu wa KKKT akiwa na mwenyeji wake Askofu wa Dayosisi ya Kusini
Msaidizi wa Askofu akiwa Mtaa wa Malangamilo

Chanzo cha Wazo la Uinjilisti
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kusini alieleza kuwa wazo la kufanya Uinjilisti alilipata mwaka jana (2024), alipokuwa akitimiza miaka 30 tangu kubarikiwa kuwa mchungaji. Alitamani kusherehekea hatua hiyo kwa njia ya kiroho, kwa kueneza Injili badala ya kufanya sherehe ya kawaida. Hata hivyo, kutokana na ratiba kuwa ngumu, shughuli hiyo iliahirishwa mwaka jana. Mwaka huu, 2025, wazo hilo hatimaye lilitimia kwa mafanikio makubwa, na likawa baraka kwa watu wengi.

Tazama Askofu akizungumza: bonyeza hapa https://youtu.be/bpkrPlh8b_0?si=qLrA7DOWnhLAUL-6

Kipekee shughuli hii iliongozwa na kuratibiwa na Mchungaji Chengula na imehusisha zaidi ya watumishi 120 kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo wachungaji, wainjilisti, pamoja watumishi wengine waliowekwa wakfu kwa kazi ya kulihubiri Neno la Mungu, kuombea jamii, na kushirikiana nao katika mahitaji ya kiroho na kijamii. Katika kipindi chote cha huduma, watumishi hawa wamefikia zaidi ya mitaa 70, wakishiriki huduma mbalimbali kwa moyo wa upendo, uvumilivu, na kujitoa bila masharti.

Watumishi wakipokea maelekezo kutoka kwa Mratibu wakiwa Mbeya
Mratibu wa shughuli ya Uinjilisti Mchungaji Isaac Chengula akitoa maelekezo kwa watumishi

Safari ilianza tarehe 01/08/2025 kukiwa na misafara kadhaa ikiwepo msafara kutoka Njombe – Makambako – Chunya, msafara kutoka Njombe – Kidugala – Ilembula – Chimala – Chunya ukiongozwa, Msafara kutoka Chimala –Chunya, msafara wa Ofisi kuu, msafara wa Ofisi ya la Chimala, msafara wa watumishi kutoka huduma ya Here is Life, msafara kutoka Dar es Salaam – Chunya.

Maeneo ya Huduma
Huduma ilifanyika katika vijiji na miji ya Jimbo la Chunya, ambako kwakweli mahitaji ya kiroho na miundombinu ya makanisa yalibainika kuwa makubwa.

Mtaa wa Upendo Usharika wa Mtande
Mtaa wa Bitimanyanga Usharika wa Sangawana

Shughuli Zilizofanyika

  • Mahubiri ya Injili katika mikutano ya hadhara
  • Maombezi na huduma ya uponyaji
  • Mafunzo ya Neno la Mungu kwa waumini wapya
  • Ubatizo wa waumini wapya
  • Kufungisha ndoa
  • Kuweka mawe ya msingi kwa ajili ya ujenzi wa makanisa, ofisi na uzinduzi wa nyumba
  • Ujenzi wa makanisa na miundombinu mingine katika kanisa
  • Ushuhuda wa waliopokea wokovu
  • Wito wa uchangiaji wa bati za kuezeka makanisa mbalimbali
  • Wito wa kibinafsi kwa kila Mkristo kufanya Uinjilisti – Mkuu wa KKKT alisisitiza kuwa kila Mkristo anapaswa kushiriki katika kazi ya Injilisti kwa kutafuta angalau waumini wapya wawili

Kutazama baadhi ya watumishi walioamua kujenga kanisa: bonyeza hapa https://youtu.be/OdhRU-S7s0k?si=hdtIh-HtgzWDhQqZ

Mchungaji Chengula akibatiza katika sharika za Matundasi
Mkuu wa KKKt baada ya kuweka jiwe la msingi mtaa wa Upendo Usharika wa Mtande
Moja kanisa lililojengwa mtaa wa Malangamilo
Huduma ya ubatizo mtaa wa Kasisi sharika za Makongolosi

Baraka za Mkuu wa KKKT
Jambo nzuri zaidi katika huduma hii ya uinjilisti, mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Daktari Alex Gehazi Malasusa alishiriki moja kwa moja kwa takribani siku 4, kuanzia tarehe 04/08/205 hadi 07/08/2025. Mkuu wa KKKT alifanikiwa kutembelea jumla ya mitaa 9; na katika ziara yake hiyo alifanikiwa kuweka mawe ya msingi kwa ujenzi wa makanisa, ofisi za sharika.

Daktari Alex Gehazi Malasusa Mkuu wa KKKT

Maeneo ambayo Mkuu wa KKKT alitembelea ni pamoja na mtaa wa Chunya, mitaa ya Kambikatoto na Bitimanyanga (Usharika wa Sangawana), mtaa wa Upendo (Usharika wa Mtande), mtaa wa Makongolosi, mitaa ya Sarepta, Miembeni na Patamela (Usharika wa Mkwajuni St. ya Saza), na mtaa Kanga (Usharika wa Kanga).

Mahali pote alipopita ujumbe mkuu wa Mkuu wa KKKT ulikuwa ni shughuli ya uinjilisti kwa kila msharika. Akizungumza katika maeneo mbalimbali alieleza kuwa mpango wa kanisa ni kuongea idadi ya waumini. Hivyo basi, kila msharika ajitahidi kutafuta, kuwahubiria na kuwavuta angalau watu wawili wajumuike nasi kanisani.

Kutazama Mkuu KKKT akizungumza: bonyeza https://youtu.be/5gf0VJlyfNQ?si=Z-zFJJkbtrtXj-Rl

 

Vijana waendesha pikipiki waliojitoa kumpokea mkuu wa kanisa

 

Wachungaji ambao pia ni wakuu wa ma kutoka Dayosisi ya Mashariki na Pwani walimsindikiza mkuu wa kanisa

Ujumbe wa Viongozi
“Kila Mkristo anapaswa kuwa mwinjilisti. Ikiwa kila mmoja wetu atatafuta angalau Wakristo wapya wawili, tutakuwa tumetimiza agizo la Bwana wetu Yesu Kristo kwa vitendo.” – Mkuu wa KKKT

“Nilitamani kusherehekea miaka 30 ya huduma kwa njia ya Uinjilisti, si kwa sherehe ya kawaida. Ninamshukuru Mungu kwa kutimiza wazo hili mwaka huu.” – Askofu wa Dayosisi ya Kusini

“Niwapongeza na kuwashukuru watumishi wote kwa kujitoa kwa moyo. Ni wakati sasa kwa watu kutoka sehemu mbalimbali kushiriki baraka za uchangiaji wa bati na ujenzi wa makanisa.” – Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi ya Kusini

Kutazama Msaidizi wa Askofu akizungumza: bonyeza  https://youtu.be/DyA8JgUhyRo?si=nJrmYVoYJ7NrknRR

Mpango wa Mwaka kwa Wiki ya Uinjilisti
Katika hotuba yake ya kufunga huduma, Askofu wa Dayosisi ya Kusini aliahidi kuwa kutokana na mafanikio ya huduma hii, “Wiki ya Uinjilisti” itakuwa tukio la kila mwaka litakalofanyika kila mwezi Agosti.

“Kwa kuwa jambo hili limeonekana ni jema, basi kila mwaka hasa mwezi August tutakuwa na shughuli hii ya Wiki ya Uinjilisti.” – Askofu wa Dayosisi ya Kusini. Ahadi hii inalenga kuendeleza ari ya Uinjilisti, kuimarisha huduma za makanisa, na kuendeleza ushirikiano wa kiroho miongoni mwa waumini.

Mapendekezo

  • Kuandaa huduma za Uinjilisti kwa muda mrefu zaidi
  • Kuendeleza kampeni ya uchangiaji wa bati hadi makanisa yote yaweze kuezekwa
  • Kuongeza mafunzo kwa watumishi wa huduma
  • Kuimarisha rasilimali za huduma
  • Kuweka mikakati ya kufuatilia utekelezaji wa wito wa kibinafsi wa Uinjilisti
  • Kuandaa kalenda rasmi ya “Wiki ya Uinjilisti” kila Agosti kwa ushirikiano wa Dayosisi nzima

Washiriki Muhimu

  • Mkuu wa KKKT
  • Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kusini
  • Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi ya Kusini
  • Watumishi wa Mungu zaidi ya 120 kutoka mikoa na ma mbalimbali

Hitimisho

Kazi ya Uinjilisti Jimbo la Chunya ilikuwa ya kipekee, ikigusa maisha ya watu kiroho na kijamii. Ushiriki wa viongozi wa juu wa KKKT ulileta msukumo mkubwa, na huduma hii imeacha alama ya kudumu. Tunamshukuru Mungu kwa matunda ya huduma hii, kwa kutimiza wazo la Askofu, na kwa kuzindua rasmi Wiki ya Uinjilisti kama tukio la kila mwaka.

Kutazama majumuisho ya Uinjilisti: bonyeza hapa https://youtu.be/LCfEvbcKSAA?si=HLIckpyxfdeteldh

 

Kwa mawasiliano zaidi:

Ofisi ya Habari na Mawasiliano
KKKT Dayosisi ya Kusini
📞 Simu: +255 769 628 082
📧 Barua pepe:
🌐 Tovuti:

 

 

 

 

Tembeza hadi Juu